22 Novemba 2012 - 20:30

Jeshi la Israel lilivunja makubaliano ya kusitisha vita wakati walipouwa Mpalestina mmoja leo ukanda wa Ghaza.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)-ABNA- Televisheni ya AL-ALAM  iliripoti habari muhimu baada tu ya kukubaliana kusitisha mapigano baina ya Israel na Palestina, Wanajeshi wa Israel waliuwa Mpalestina mmoja katika maeneo ya Khan Yusuf, na alieuawa ni Anwar Qadih.

Kulingana na ripoti hii baada ya kupiga risasi na kujeruhiwa watu kadhaa televisheni hii iliripoti haraka habari hii.

Aidha katika kuvunja makubaliano hayo leo hii walishikwa wabunge kadhaa wa Palestina walokuwa wakielekea Jordan.